Akitoa salamu kwa wananchi wa Iringa katika maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani amesema, Maadhimisho haya yamekuwa yakifanyika kila mwaka duniani kote, pia inatoa fursa ya kukumbushana juu ya janga hili la UKIMWI. Haya ameyasema Mheshimiwa Jamhuri David William (Mkuu wa Wilaya ya Mufindi) ambaye alikuwa Mgeni Rasmi akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa Mheshimiwa Ally Hapi katika maadhimisho hayo.
Nimefarijika kwa uwepo wenu na kushirikiana katika mapambano dhidi ya UKIMWI, Wana Iringa ni ukweli kuwa, kila mmoja wetu ni muathirika kwa namna moja au nyingine, hivyo kwa nini tusiwajibike kwenda kupima? Tukipima tutajua hali zetu na tukiwa na maambukizi tutatumia dawa , hivyo kuendea kufanya shughuli zetu.
Bado tuna changamoto za unyanyapaa, ukosefu wa usiri kwa watoa huduma, pia watu kujitokeza kwenda kupima pale wanapohisi wanaumwa tu, na umbali wa kwenda kutafuta hutafuta huduma. Suala la kupima na kuanza kutumia dawa mapema litapunguza kasi ya maambukizi mapya na kuimarika afya.
Kupitia maadhimisho haya, nawaagiza Mganga Mkuu wa Mkoa, Waganga Wakuu wa Halmshauri na watoa huduma wote kuendelea kufanya kazi pamoja ili kufikia malengo ya 90-90-90 kw mwaka 2020. Pia nawaagiza Wakuu wa Wilaya zote za Mkoa wa Iringa kusimamia hospitali kutoa kwa kutoa huduma bora za afya.
Nampongeza Katibu Tawala wa Mkoa Mheshimiwa Happiness Seneda kwa kuandaa maadhimisho haya, pia wadau na wanchani kwa kuonesha bidhaa mbalimbali.
Kauli Mbiu katika Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI kwa mwaka huu 2019 ni “Jamii ni Chachu ya Mabadiliko Tuungani kutokomeza Maambukizi ya VVU”.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Telephone: +255 262 702 715
Mobile:
Email: ras@iringa.go.tz
Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.