Salamu za Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimiwa Ally Hapi katika Mazishi ya Aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria Mheshimiwa Balozi Dr. Augustine Philip Mahiga Yaliyofanyika Nyumbani Kwao Kijiji cha Tosamaganga Mei 02, 2020
Mheshimiwa Mahige amefariki Mei o1, 2020 baada ya kupata homa ya ghafla huko Dodoma.
Kabla ya kutoa salamu zake za pole Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimiwa Ally Hapi alimkaribisha Jaji wa Mahakama Kuu Tanzani Iringa Mheshimiwa Pentelini Kente kutoa salamu zake za pole. Akafuatia Dr. Tulia Ackson Mheshimiwa Naibu Spika wa Bunge la Tanzania naye kutoa salamu zake za pole na jinsi alivyoagizwa salamu kutoka kwa Mheshimiwa Job Ndugai Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akitoa salamu za pole kwa ndugu, familia na wanairinga kwa ujumla, Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimiwa Hapi alianza kwa kumshukuru Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu kwa kuja kuungana nasi katika msiba huu mzito na pia kwa kumuwakilisha Rais wa Tanzania Mheshimiwa John Pombe Magufuli.
Akiongea kwa masikitiko Mheshimiwa Hapi amesema, tumepata pigo kubwa sana. Sisi kama viongozi vijana tunajifunza kutoka kwake kuwa alikuwa mnyenyekevu, mcheshi na asiyependa makuu na alimsikiliza kila mtu na hakuweza kujikweza. Ukisikiliza wasifu wake kuna hana ya kutunga kitabu kwa ajili yake ili vijana tuweze kusoma na kujifunza kile alichokiishi kiongozi huyu. Natoa pole kwa familia na Iringa kwa ujumla kwa kumpoteza kiongozi mahiri mzee wetu.
Baada ya kutoa salamu hizo Mheshimiwa Hapi alimkaribisha Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu naye kutoa salamu zake za pole. Mama Suluhu amesema, nimesimama hapa kwa niaba ya Mheshimiwa Rais naye ameleta pole kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Wizara pia kwa familia na Iringa. Tumeondokewa na mpendwa wetu Waziri mwenye uzoefu, kwani marehemu alikuwa anawakilisha Kitaifa na Kimataifa na kuimarisha ushirikiano, alimaliza kusema Mama Suluhu.
“Bwana Alitoa, Bwana Ametwaa, Jina la Bwana Lihimidiwe, Aamina! “
Imetolewa na:
Ofisi ya Habari Mkoa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Telephone: +255 262 702 715
Mobile:
Email: ras@iringa.go.tz
Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.