Mkuu wa Mkoa Mheshimiwa Ally Hapi Amepokea Vifaa Kinga vya Kujikinga na Maambukizi ya Ugonjwa wa Covd-19 Kutoka kwa Wadau Mbalimbali tarehe 29/04/2020
Akitoa hotuba fupi ya tukio hilo Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa amesema, tuko katika mapambano dhidi ya maambukizi ya covid-19, tuna mambo ya kuzingatia juu ya kujikinga na maambukizi. Kwa mujibu wa Mheshimiwa Waziri Mkuu watu zaidi ya 400 wameambukizwa, pia matumaini yapo kwa wagonjwa zaidi ya 100 wamepona ugonjwa huu na kuruhusiwa kutoka hospitali.
Pia anawaasa wananchi wanaotoa masomo ya ziada kimyakimya kuwa wakibainika watachukuliwa hatua wazazi na watoa masomo hao.
Mkuu wa Mkoa amesema pia katika mazishi watu hawazingatii kukaa umbali wa mita moja kutoka mtu mmoja hadi mwingine, hii itasababisha kuongeza maambukizi haya.
Mkuu wa Mkoa ametoa maagizo kwa Katibu Tawala kuwa, aongee na viongozi wa dini ili kuzingatia tahadhari hii, kwani ugonjwa huu upo na ni hatari sana.
Jeshi la Polisi na Mamlaka za Mitaa nawaagiza kufuatilia wananchi ambao hawachukui tahadhari. Mwananchi yeyote anayekuja kupata huduma katika Ofisi za Umma lazima avae barakoa. Pia amesisitiza kuwa, huu siyo wakati wa kutembeleana bila sababu, nitoe rai kwa wananchi tusisafiri bila sabab za msingi.
Ameongeza kusema kuwa, kuna baadhi ya wafanyabiashara kutokana na maambukizi haya, wamepata fursa ya kuongeza bei kwa bidhaa na chakula kama sukari. Na sasa tupo katika kipindi hiki cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani siyo vizuri kufanya hivyo, kwani Serikali imetoa bei elekezi hivyo kama umeongeza bei yako lazima utakamatwa.
Nachukua nafasi hii kuwashukuru wadau wetu ambao wametusaidia kutupatia vifaa mbalimbali vya kujikinga na maambukizi haya hasa kwa hawa watoa huduma. Vifaa hivyo ni kama magauni, vitakasa mikono, sabuni, matanki kwa ajili ya maji, barakoa na vipima joto. Wadau hao ni ASAS, Sai Villa, Qwihaya, Clinton Foundation na wengine wengi waliojitoa kwa ajili ya kupambana na gonjwa hili hatari kwa jamii, nasema tena ahsanteni sana kwa kutuunga mkono.
Mkuu wa Mkoa alimaliza kwa kusema, natoa rai kwa wananchi wanaotoa taarifa za upotoshaji kuhusu ugonjwa wa Corona, nafurahi kuona Jeshi la Polisi lipovizuri katika kuwafuatilia watu hawa na kuwachukulia hatua, nawapongeza sana, endeleeni kufanya kazi vizuri kwa weledi.
Pia Mheshimiwa Hapi ameendelea kuwasisitiza wananchi kuchukua tahadhari juu ya Covid-19.
Imetolewa na:
Ofisi ya Habari Mkoa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Telephone: +255 262 702 715
Mobile:
Email: ras@iringa.go.tz
Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.