Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Isdori Mpango amemkabidhi funguo ya gari na Cheti Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimiwa Peter Serukamba baada ya Mkoa wa Iringa kuibuka Mshindi wa Jumla wa Usafi wa Mazingira na Ujenzi wa Vyoo Bora(ODF) kwa mwaka 2023.
Zawadi hiyo imetolewa kwenye uzinduzi wa Kampeni ya Mtu ni Afya Awamu ya Pili iliyofanyika uwanja wa Stendi ya mabasi ya zamani ya Maili moja Mji Kibaha Mkoani pwani na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali, Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Waheshimiwa Madiwani , Wakurugenzi na wakuu wa Idara na Wananchi Mbalimbali.
Akizungumza wakati wa kuzindua Kampeni hiyo Mgeni Rasmi Ambae ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango amesema Kampeni hii inahimiza kila mwananchi ajikinge na maradhi na kupunguza gharama kwa Serikali kwa Mikakati Tisa:-
- Ujenzi wa vyoo bora kwenye maeneo yote ya mikusanyiko
- Kunawa mikono kwa maji tiririka
- Uondoshaji wa maji taka
- Kutibu maji ya kunywa
- Hedhi salama kwa watoto wa kike
- Menejimentiti ya taka mgumu
- Lishe bora
- Usafi wa mazingira
- Elimu kuhusu tabia nchi na nishati bora ya kupikia
Mkoa wa Iringa umepata Ushindi wa Jumla wa Usafi wa Mazingira na Ujenzi wa Vyoo Bora (ODF) 2023 ambapo ni ushindi wa Halmashauri zote za Mkoa wa Iringa na umekabidhiwa gari landcruser na cheti . Hafla imehudhuriwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Comrade Daudi Yassin,
Kuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Dkt. Linda Salekwa, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga Mhe. Regnant Kivinge na Wakuu wa Idara wa Afya na usafi wa Mazingira na watendaji wa Kata.
Kauli mbiu: Mtu ni Afya
Afya yangu wajibu wangu
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Telephone: +255 262 702 715
Mobile:
Email: ras@iringa.go.tz
Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.