Mkuu wa mkoa wa Iringa Mhe.Queen Sendiga ameonyesha kufurahishwa na matumizi mazuri ya fedha za mpango wa kunusuru kaya masikii (TASAF) katika wilaya ya Mufindi, ameyasema hayo wakati akifanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na mfuko huo.
Katika ziara hiyo mkuu wa Mkoa amekagua shamba la miti ya maparachichi katika kijiji cha Ikanga, shamba la miti, matunda na miti ya maparachichi katika kijiji cha ludilo ambavyo vinapatikana katika kata ya Mdabulo wilayani Mufindi mkoani Iringa.
" Nimefurahishwa sana na jinsi fedha zilivyotumika vizuri kwa kulima Parachichi mtaongeza kipato chenu endapo kila familia moja katika kijiji ikilima ekali moja ya parachichi tutaongeza kipato katika familia zetu mti mmoja wa parachichi endapo tutatunza vizuli tutapata si chini ya laki tatu ndani ya mwaka ". Mhe. Queen Sendiga
Aidha Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Saad Mtambule ametoa pongezi zake kwa utekelezaji mzuri wa miradi hiyo kwani inawapanguzia ugumu wa maisha wananchi kwa kuwapa fursa ya kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Telephone: +255 262 702 715
Mobile:
Email: ras@iringa.go.tz
Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.