Mkuu wa Mkoa Mh. Queen Sendiga amefanya Uzinduzi wa chanjo ya polio Mkoani Iringa Leo Hii tarehe 18/5/2022 ndani ya kambi jeshi la Magereza Iringa, ambapo ametembea nyumba kwa nyumba kuzindua chanjo hiyo ya polio , katika uzinduzi huo aliongozana na Katibu Tawala Mkoa Bi Happiness Seneda pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe Mohammed Moyo .
Pia Mkuu wa Mkoa amewataka wananchi wajitokezee kwa wingi na kutoa ushirikiano Mkubwa kwa wahudumu wa afya wanaotoa chanjo hiyo ya polio ,hivyo chanjo hiyo inatolewa kwa watoto wenye umri chini ya Miaka 5.
Akito taarifa hiyo Mganga Mkuu wa Mkoa Daktari Mohamed Mang’ung’a amesema kuwa ‘’ Chanjo ya ugonjwa wa polio inatalajia kufikia watoto jumla 168,658 Pia Mkoa wa Iringa umepokea jumla ya dozi 193,960 ya chanjo ya polio na droppers 193,960’’
Jumla ya Vituo 254 vitakavyo toa huduma ya chanjo ya polio Vituo Ivyo Hospitali 9, Vituo vya afya 29 na Zahanati 216 ndani ya Halmashauri ya Iringa DC, Mufindi DC, Iringa MC, Kilolo DC,Mafinga TC na Iringa
Mhe. Queen Sendiga amesema chanjo iyo itasaidia kuwakinga watoto na ulemavu lakini itapelekea kuongeza kinga kwenye mihili ya watoto.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Telephone: +255 262 702 715
Mobile:
Email: ras@iringa.go.tz
Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.