Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa
Watendaji wilayani Kilolo wametakiwa kuwafuata wananchi katika maeneo yao na kutatua kero zao ili wafurahie uwepo wa serikali iliyopo madarakani.
Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe Ally Hapi alipokuwa akiongea na wazee wa Wilaya ya Kilolo katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya Wilaya ya Kilolo jana.
Mhe Hapi alisema “nimewaagiza watendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Kilolo kuwafuata huko mlipo na kutatua kero zenu, siyo nyie kuja kuwafuata watendaji walipo”. Sitaki kusikia mnakero na watendaji hawajafika kuzitatua, aliongeza Mhe Hapi. Alisema kuwa aliamua kuanza kikao cha kazi na watendaji wa wilaya hiyo ili kuwapa maelekezo na dira anayoitaka katika kuwahudumia wananchi. Aliongeza kuwa kana wakati wananchi wanaichukia serikali yao kutokana na utendaji kazi wa watendaji usio wa kuridhisha.
Mkuu wa Mkoa aliwaambia wazee hao kuwa ameenda kujitambulisha Wilayani Kilolo. Baada ya kunipokea nitafanya ziara ya tarafa kwa tarafa kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia majawabu, hii ndiyo Iringa mpya ninayoitaka ambayo wananchi wake hawana kero, alisisitiza. Aidha, aliwaomba wazee wa hiyo kumpa ushirikiano katika kutekeleza majukumu ya serikali na kuiunga mkono serikali yao.
Mkuu wa Mkoa amefanya ziara yake ya kwanza katika Wilaya ya Kilolo kujitambulisha kwa Chama cha Mapinduzi, kuongea na watumishi, wazee na kufanya mkutano wa hadhara.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Telephone: +255 262 702 715
Mobile:
Email: ras@iringa.go.tz
Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.