Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe, Queen Sendiga, leo ameongoza kikao kazi cha tathimini ya mradi wa Tasaf kilichofanyikia katika ukumbi wa Halmashauri ya Mufindi.
Mhe, Queen Sendiga (RC) akifungua kikao hicho amempongeza Katibu Tawala Mkoa na timu yake kwa kazi nzuri sana wanayofanya kwenye kila eneo inapelekea kuwa na ufanisi mkubwa na tija kwa Mkoa.
Hata hivyo Mhe Sendiga, amemuagiza Mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe, Mohamed Moyo Kwa kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kufanya utafiti wa wazee wanaozunguka mitaani mjini Iringa na kukaa kwenye mageti ya watu na kuomba kuona kama wapo kwenye mpango kunusuru kaya masikini Tasaf na kama hawapo basi waweze kuingizwa kwenye mpango huo.
Mhe, Mkuu wa Mkoa Sendiga, metoa agizo hilo Leo akiwa Mafinga wakati wa Kikao kazi cha tathimini ya Kipindi cha Pili cha TASAF awamu ya tatu cha miaka minne kuanzia 2020 – 2023.
"Nimepata kuzunguka maeneo mbali mbali ya wilaya ya Mufindi na Kilolo nimeona jinsi mpango huu wa TASAF ulivyonufaisha walengwa kuwa na miradi mizuri na yenye tija kubwa hivyo ni furaha yangu kuona walengwa Kama awa wanahitimu.
Hata hivyo aliagiza watendaji wa mitaa na vijiji pamoja na Viongozi wengine kutoka maofisini na kwenda Kwa walengwa ili kuendelea kuwapa elimu ya matumizi sahihi ya fedha za TASAF Kwa kuzitumia fedha vizuri badala ya kutumia fedha hizo kunywea pombe .
Mhe Sendiga, amesema kuwa anafurahishwa sana mpango wa TASAF Ndani ya Mkoa wa Iringa umekuwa na mafanikio makubwa sana kutokana na walengwa kuwa na mafanikio makubwa ya kimaendeleo jambo ambalo linaonesha wazi mpango huo kuwa na faida .
"Natamani kuona wataalamu wa Kilimo na Mifugo wakatoka ofisini na kwenda Kwa walengwa kuwapa elimu ya Kilimo na ufugaji itasaidia walengwa wa TASAF kufanya shughuli zao kisasa zaidi ".
Mhe Sendiga, ametoa agizo kwa wakurugenzi kushirikiana na waratibu wa mpango huo wa TASAF ili kuleta tija zaidi na siyo wanakuwa mbali hii inapelekea baadhi ya watendaji wasio wahaminifu wanatumia mwanya huo kuweka majina ya wanufaika wasio sahihi, pia kuweka utaratibu mzuri kwenye shule ili kusaidia kupata mahudhurio ya wanafunzi wanaonufaika na fedha hizo za Tasaf tofauti na sasa kumekuwa na ucheleweshaji wa mahudhurio hayo hivyo wamchague mtu mmoja kwa kila shule atakekuwa anasimamima kazi hiyo.
Nae Katibu tawala wa mkoa wa Iringa Bi, Happiness Seneda (RAS) amesema kuwa lengo la kufanya kikao kazi hicho ni kujenga uelewa wa pamoja juu ya mpango huo wa kuondoa Umaskini kwa kaya zenye hali duni sana, lakini pia kujua changamoto zake zinazopelekea kukwamisha baadhi ya maeneo kutofanya vizuri.
"Kumekuwa na changamoto kubwa hasa katika mfumo wa ukataji rufaa za wanufaika hivyo naomba mtusaidie ninyi wa makao makuu ya Tasaf, Pia Kuna changamoto ya mfumo wa ulipaji ususani kwa wazee hii inapelekea kuibiwa fedha zao na wajukuu zao kwa sababu ya kuto jua tumia simu vizuri "
Bi, Happiness Seneda (RAS) amewataka waratibu wa Tasaf kuhakikisha wanajipanga vizuri wakati ujuao na kuja na taarifa iliyokuwa na mpangilio mzuri na walete changamoto ngumu ambazo kweli zinatakiwa zijadiliwe kwenye kikao hicho.
" Hata hivyo nitumie fursa hii kuwa pongeza kwa kazi nzuri mnyaofanya waratibu wa Tasaf wote, nawataka kuendelea kuhakiki majina ya wanufaika vizuri.
Katika kikao hicho alihudhulia Mhe Mwenyekiti wa CCM Mkoa Dr, Abel Nyahanga, na Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya ya Iringa Mhe Mohamed Moyo, na Mhe Saad Mtambule Mkuu wa Wilaya ya Mufindi.
Imetolewa na Afisa habari Mkoa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Telephone: +255 262 702 715
Mobile:
Email: ras@iringa.go.tz
Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.