Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba ametoa masaa 24 Kwa wafanyabiashara wanaomiliki vibanda katika soko la Mafinga kuvunja vibanda 331 vilivyojengwa kimakosa katika eneo linalomilikiwa na Halmashauri ya Mji Mafinga ambavyo husababisha hasara ya zaidi ya Millioni Kumi Kwenye Halmashauri hiyo.Hayo yamejiri wakati alipofanya ziara ya ukaguzi katika soko hilo akiwa ameambatana na kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya na MkoaMhe. Serukamba amesema kuwa Halmashauri haiwezi kuendelea endapo hakuna mapato yoyote yale yanayoingia katika Halmashauri hivyo amesema kuwa hawajalipa kodi kwa zaidi ya miezi sita basi wapishe kwenye eneo hilo la Halmashauri Hivyo amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kwanza kuzungushia utepe kwenye eneo hilo ili vibanda hivyo viweze kubomolewa."Kwahiyo nimetoa maelekezo watakuja kufunga liboni tanesco wataondoa umeme ili kesho kutwa tunaanza kubomoa vibanda vyote ili tubakie na ardhi yetu halafu baada ya hapo tutajua tunalipangaje soko letu na tutaanza kufanya biashara na wale ambao watahitaji kufanya biashara na sisi"Nae Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Dkt. Linda Salekwa amesema kutokana na kukosa Mkataba wafanyabiashara hao wamekosa leseni na kupelekea Halmashauri hiyo kukosa mapatoKwa upande mwingine Mkuu wa Idara ya Viwanda na Biashara wa Halmashauri ya Mji Mafinga Ndg. Evance Mtikile suala la mgogoro wa mkataba kati ya wafanyabiashara hao na Halmashauri limeanza tangu mwaka jana ambapo wafanyabiashara wamekuwa wakigomea mkataba huo na kupelekea Halmashauri hiyo kukosa mapato.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Telephone: +255 262 702 715
Mobile:
Email: ras@iringa.go.tz
Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.