Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba amemuagiza Katibu Tawala na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kukutana na Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijajini na Mijini TARURA kuzungumza nae kwaajili ya Ujenzi wa barabara iendayo katika kituo cha Afya cha wenda kinachomilikiwa na kanisa la Katoliki Jimbo la Iringa.
Hayo yamejiri wakati aliposhiriki katika uzinduzi wa jengo la upasuaji mkubwa lililopo katika kituo hicho.
Akitoa taarifa ya kituo hicho mganga mfawidhi wa kituo hicho Sister Sabina Mangi amesema ujenzi wa jengo hilo mpaka kukamilika kwake ni zaidi ya Millioni Mia sita zimetumika kukamilisha jengo hilo wakati ununizi wa vifaa umegharimu kiasi cha shilingi Milioni Mia Mbili Tisini na Tano, ambapo amesema jengo hilo limeleta ukombozi kwa akina mama kwani kwa sasa wanafanyiwa upasuaji wa dharura na upasuaji wa kawaida katika kituo hicho.
Pia ameongeza kwa kusema mbali na mafanikio hayo lakini wanakumbana na changamoto ya miundombinu mibovu ya barabara ambapo wameiomba serukali iweze kuwasaidi mita 900 za barabara
Akizungumza katika hafla hiyo Mhe. Serukamba amepongeza jitihada kubwa zinazofanywa na taasisi za kidini kwa kutoa huduma za kijamii huku akiahidi na kuagiza kwa watendaji kuhakikisha wanakaa na kujadili na TARURA namna watakavyoondoa changamoto ya barabara inayoelekea katika kituo hicho.
"Nitoe Maagizo kwa Katibu Tawala wa Mkoa, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa mumlete mtu wa TARURA aje aangalie aone tunafanya nini kuboresha barabara hii"
Nao baadhi ya wananchi wametoa shukrani nyingi sana kwa serikali na kanisa kwa kukiendeleza kituo hicho tangu kilipoanza mpaka sasa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Telephone: +255 262 702 715
Mobile:
Email: ras@iringa.go.tz
Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.