Wanafunzi Mkoani Iringa waishukuru Serikali kwa kuwajengea mabweni yatakayo wasaidia na kuepusha adha ya kutembea umbali mrefu jambo ambalo linafanya kukosa baadhi ya vipindi darasani na muda wa kujisomea.
Hayo yamebainishwa leo October,22,2024 wakati wa Ziara ya ukaguzi wa Miradi iliyo ongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa
Wakizungumza katika ziara hiyo baadhi ya wanafunzi wameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuwaondolea adha ya wao kutembea umbali mrefu huku wakiahidi kuendelea kufanya vizuri katika masomo yao
"Kukota hapa mpaka huko nduli ni kilometa 4 lakini kutoka hapa mpka Nyumbani ni kilometa 8 kutoka hapa shule huwa tunatoka saa11 Nyumbani tunaweza kufika hata Saa 2 kwahiyo wanakosa hata muda wa kujisomea maana wakifika nyumbani wanakutana na kazi nyingi."
Akikagua miradi hiyo Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba amesema kuwa jukumu la Serikali ni kuhakikisha miradi yote inaisha kwa wakati ifikapo Tarehe 30 Novemba.
Naye mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada amesema kuwa jukumu la ujenzi wa mabweni hayo ni kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata elimu katika mazingira rafiki yatakayowafanya wao kupata Elimu bora na uwezo wa wanafunzi kielimu unapanda.
Muongoni mwa miradi aliyoikagua ni ujenzi wa bweni la shule ya sekondari Nduli ambapo ujenzi wake umegharimu zaidi ya Million 26.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Telephone: +255 262 702 715
Mobile:
Email: ras@iringa.go.tz
Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.