Wanafunzi waliopo katika kata ya Ulanda tarafa ya Kalenga katika Halmashauri ya wilaya ya Iringa wanatarajia kuondokana na adha ya kutembea umbali mrefu wa Km 13 kwenda kupata masomo katika shule ya Sekondari ya Kalenga.
Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuboresha na kuongeza miundombinu ya Elimu ambapo imemwaga zaidi ya Tsh. Millioni Miatano za ujenzi wa Shule ya sekondari ya Weru katika kata hiyo.
Wakizungumza na Mkuu wa Mkoa Viongozi na wananchi wa kata ya Ulanda wametoa pongezi nyingi sana kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kusikia kilio chao na kutoa fedha nyingi za ujenzi wa shule ambapo wamesema uwepo wa shule hiyo utaleta maendeleo katika taifa hili kwani wanafunzi kwa sasa ile adha waliokuwa wakikumbana nayo ya kutembea umbali mrefu kwenda kupata masomo itakuwa imekwisha hivyo watasima katika mazingira mazuri na kufaulu.
Ikumbukwe kuwa eneo shule hiyo ilipojengwa ni eneo ambalo familia ya mzee Sambala imejitolea bure ili ijengwe shule hiyo jambo ambalo limemfurahisha mkuu wa mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego ambapo amewashukuru sana wanafamilia kwa kujitoa kwao kwa moyo mweupe pasipo kuwa na tatizo lolote.
Hivyo basi Mhe. Dendego ameuagiza uongozi wa Halmashauri hiyo kwenda kubadirisha jina la usajili wa shule hiyo na kwamba shule hiyo iitwe Sambala ili kuienzi familia iliyojitolea eneo hilo.
Hii ni ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi katika mkoa huo ikiwemi miradi ya kuboresha shule za sekondari SEQUIP awamu ya Pili.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Telephone: +255 262 702 715
Mobile:
Email: ras@iringa.go.tz
Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.