Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego amewataka vijana nchini kuwa wazalendo kwa kuyatangaza mazuri yote yanayofanywa na Serikali.
Ameyasema hayo wakati wa kongamano la kumpongeza Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania kwa kazi anazozifanya lililoandaliwa na Umoja wa Wananfunzi wa Vyuo Vikuu CCM Mkoani Iringa.
Mhe. Dendego amesema kuwa vijana ndio nguvu kazi na taifa liweze kusonga mbele na kuwa na mandeleo linahitaji vijana wenye nguvu na wazalendo katika nchi yao hivyo amewasisitiza wanafunzi hao kusoma kwa bidi na kuisemea vyema Serikali kwa mambo makubwa inayoyafanya ikiwemo uboreshaji wa Miundombinu na utoaji wa Huduma nzuri kwa Wannchi wake.
Pia Mhe. Dendego ameongeza kwa kutoa rai kwa Wanafunzi hao kufanya juhudi katika kujikinga na maambukuzi ya virusi vya UKIMWI na kusema kuwa wao ndio nguvu kazi ya Taifa hivyo wanatakiwa kufanya kazi kwa bidi na kujiepusha na ngono zembe.
Akitoa salaamu za Chama Cha Mapinduzi Mwenezi wa CCM Mkoa wa Iringa Ndugu Joseph Lyata humo amewasisitiza Wanafunzi hao kutumia vyema Teknolojia kwa kutangaza utamaduni wa Kitanzania na yale yote yanayofanywa na Serikali.
Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Telephone: +255 262 702 715
Mobile:
Email: ras@iringa.go.tz
Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.