Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi .Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima ametoa siku 14 kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii nchini kuwasilisha taarifa ya ushirikishwaji wa wafanyabiashara ndogondogo yaani Machinga kuhusu mfumo wa usajili wa Machinga.
Dkt. Gwajima ametoa agizo hilo wakati akizungumza kwa nyakati tofauti katika ziara yake mkoani Iringa.
Akizungumza katika kikao cha Wataalamu wa Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii na viongozi wa machinga Mkoani Iringa, amesema kuwa zoezi la usajili wa machinga katika mfumo wa kielektroniki uliozinduliwa na Serikali hivi karibuni, unasuasua katika mikoa yote nchini, ambapo katika kikao hicho imebainika ni kutokana na machinga kutopata taarifa sahihi kutoka kwa wataalamu.
"Natoa siku 14, nipate taarifa ya vikao vilivyofanywa na Maafisa Maendeleo ya Jamii na viongozi wa machinga kuwaeleza kuhusu utaratibu wa kujisajili vitambulisho vya machinga na nipate taarifa ya Mwenyekiti wa machinga kama ameshirikishwa" amesema Waziri Gwajima.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Telephone: +255 262 702 715
Mobile:
Email: ras@iringa.go.tz
Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.