Bi, Happyness Seneda (RAS) amefanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali katika shule ya LUGALO sekondari. Na kujione ni jinsi gani shule hizo zimejipanga ili kufaulisha wanafunzi kwa Mwaka huu.
Akisoma taarifa ya ufaulu, Mkuu huyo wa shule amesema ufaulu wastani 92% kwa kidato Cha pili.
Bi Seneda, amewashukuru kwa taarifa hiyo na kusimammia ujenzi huo, na amewataka Halmashauri ya Manispaa kutenga bajeti ili kurabati nyumba za Waalimu.
Pia amewataka kuongeza spidi hasa katika kuongeza ufaulu maana LUGALO ni shule kongwe hivyo hafurahishwi na matokeo hayo. Amekili Mwalimu Mkuu kuwa ni kweli ufaulu uko chini sana, lakini kuanzia sasa wamejipanga kwa kuanza na wanafunzi kukaa kambi na kufundisha wanafunzi. Pia na kudhibiti Waalimu ambao nao ni watoro.
Akifafanua Afisa Elimu wa Wilaya ya Manispaa Bi Tupe Kayinga Asema changamoto kubwa wanayopata sababu kwa manispaa hawana hostel kabisa hivyo kufanya utoro kuwa mkubwa zaidi. Lakini wamekubaliana mwezi 6 watakuwa na makambi kwa pamoja kwa muda wote wa likizo na wakifungua tu watafanya mthiani wa mock. Na Kuna fomu wamezianzisha maalumu kwa ajili ya kudhibiti Waalimu ili kujua Kama anafundisha vipindi vyake kwa wakati, lakini pia wamegundua tatizo la utoro linasababishwa na ukosefu wa chakula, na kila mzazi ataleta chakula badala ya mchango wa fedha.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, amesema lengo la Mkoa ni kushika nafasi ya kwanza. Amesema kumekuwa na changamoto kubwa sana hasa shule za mjini sababu Waalimu wako bize na mambo yao.
Bi Seneda (RAS) ameongea na Waalimu wa sekondari ya LUGALO na kuwapongeza kwa kazi nzuri wanayofanya hasa katika ufaulu ndani ya Mkoa wa Iringa. Lengo la ziara yake nikuendelea kuona mikakati waliyoiweka inatekelezwa ili kuongeza ufaulu. Hata hivyo amewaambia Waalimu hao kuwa bado hajaridhishwa na ufaulu katika shule hiyo ambao unapelekea kushusha Mkoa katika ufaulu huo.
Kuna changamoto sana kwa Waalimu zaidi katika utoro, upungufu wa Waalimu wa sayansi siyo sababu kubwa ni kujituma zaidi kwa Waalimu hao ili wanafunzi wafaulu vizuri. Akitoa mfano huo na kuwatia moyo Waalimu amesema hata yeye alishawahi kuwa mwalimu wa chemistry na biology lakini leo ni katibu Tawala wa Mkoa, hivyo wasikate tamaa sababu hawajui kesho yao.
Akisema mwalimu Mlilla Chigomelo amsema tatizo kubwa kupandishwa madaraja na nauli za likizo ni tatizo kubwa hii inavunja morali ya kazi.
Naye mwalimu Kasumuni, amesema kumekuwa na tatizo kubwa hasa muongozo wa kuwataka wanafunzi wenye ulemavu wa macho kusoma sayansi, wakati hawaoni future yao ya baadae, sababu masomo ni mengi sana, Na shida nyingine uhaba wa vifaa kwa watoto wenye ulemavu wa macho ambapo mpaka Sasa Wana mashine 28 tu nazo ni mbovu.
Pia amezungumzia ushirikiano kati ya Waalimu na Wazazi, maana Wazazi wamewaachia jukumu hilo la watoto Waalimu peke yao, mfano mtoto/wanafunzi wakirudi nyumbani wanaangalia tv tu na inapelekea kulala usiku sana na wanapokuwa darasani wanasinzia tu.
Pia Kuna upungufu mkubwa wa vitabu vya chemistry hivyo inawawia vigumu kuwashawishi wanafunzi kusoma sayansi.
Akifafanua juu ya changamoto hizo za Waalimu Afisa Elimu wa manispaa amesema mpaka sasa wamekwisha wapandisha madaraja na mishahara yao inarekebishwa. Kuhusu malipo ya fedha za likizo itatolewa kwa awamu kulingana na fedha wanazopata.
Akiwa shule ya sekondari ya wasichana (Iringa Girls) Bi. Seneda, amesomewa Taarifa ya maendeleo ya mradi na ufaulu wa shule hiyo.
Amepongeza sana kwa Mkuu wa shule hiyo bi Nkondola kwa kuendelea kupunguza deni la shule alilolikuta milioni 400, ambapo amekwishalipa milioni 200.
Bi Seneda, amewataka Halmashauri ya Manispaa kujenga uzio wa shule hiyo ni muhimu sana. Ambapo Katibu Tawala Mkoa naye ameahidi kuwaletea saruji( cement) mwezi wa 3.
Pia Bi. Seneda, ametembelea shule ya sekondari Tosamaganga.
Akisoma taarifa ya shule Mkuu wa shule hiyo Mwalimu Mgimwa, amesema shule inapanda kwa ufaulu na wanamkakati wa kufuta daraja la nne na 0.
Amsema ndugu Mgimwa kuwa ukarabati unaendelea ambapo mpaka sasa majengo 13 yapo kwenye hatua nzuri. Fedha iliyotumika milioni 53.
Bi. Seneda amewapongeza kwa usimamizi wa ukarabati wa majengo hayo.
Pia bi Seneda, alitakujua changamoto zao zinazopelekea kushuka kwa ufaulu, ndi Mwalimu Mkuu Mgimwa, alisema tatizo kubwa ni ukosefu wa maji kwa ajili matumizi ya wanafunzi na ukosefu wa vifaa vya sayansi kwa ajili ya mafunzo ya wanafunzi.
Hivyo bi Seneda, amemtaka mwalimu Mkuu huyo ndugu Mgimwa, kuongeza kasi sana katika ufaulu. Amemuagiza Afisa Elimu wa Wilaya ya Iringa kufatilia kwa kina juu ya shule hii, maana hakuna Mpango kazi wa ufaulu.
Bi Seneda, amewataka kuona mikakati mipya kwa ajili ya kuongeza ufaulu maana shule hii ni kongwe sana na ina historia nzuri toka zamani sasa hataki kuona historia inaharibika. Pia amewaagiza akae na Waalimu na wajue nini changamoto zao na ipi mikakati yao kwa ajili ya kuongeza ufaulu shuleni hapo.
Amewataka kutengeneza timu kazi kuanzia ngazi ya Wilaya hadi shuleni itakayoleta morali na hatimaye itasaidia kuleta ufaulu.
Imetolewa na:
Ofisi ya Habari Mkoa,
Humphrey Kisika.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.