Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe, Queen Sendinga amesema kuwa serikali ya Mkoa wa Iringa imetoa zaidi ya bilioni kwenye mfuko wa akina mama wa asilimia 4 na wamejipanga kuhakikisha mwaka ujao wa fedha wataongeza zaidi ya hapo.
Mhe, Sendiga amesema kuwa serikali ya awamu ya sita imefanikiwa kuwatua ndoo wanawake wa Mkoa wa Iringa kwa kuleta miradi mingi ya maji kwenye kila wilaya na halmashauri zake.
Amesema kuwa Iringa bado kuna changamoto ya ukatili wa kijinsia hivyo serikali ya Mkoa wa Iringa kupitia Polisi na Mahakama imeanza kushughulikia kesi za ubakaji na ulawiti na kisha kuwafunga watuhumiwa wote ambao wamekuwa wanafanya vitendo vya kikatilii.
Mhe, Sendiga amesema kuwa wananchi wa Mkoa wa Iringa waache mara moja tabia ya kuwaficha wananchi ambao wamekuwa wakifanya vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa sababu nao watashughulikiwa na serikali kama watuhumiwa wengine.
Mhe, Queen Sendiga, amezungumza hayo akiwa kwenye baraza la Wanawake la Mkoa wa Iringa ambapo pia limehudhuriwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania bi, Gaudentia Kabaka. Ambaye yupo Mkoani Iringa kwa ajili ya ziara ya siku mbili kuanzia tarehe 16-17/6/2022.
Bi, kabaka, nitumie fursa hii kuwapongeza sana Mhe Rc Sendiga na ndugu, Happynes Seneda (RAS) kwa ushirikiano wenu mkubwa wa kazi ambao unadhibitisha manafanya kazi nzuri na yenye tija kubwa ndani ya Mkoa wa Iringa, hivyo endeleni kushirikiana nasi Kama UWT Taifa tunaziona na tutawasemea vizuri kubwa endeleeni kuchapa kazi uku mkishirikiana na CCM Mkoa.
Imetolewa na Afisa habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.