Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa
Viongozi wa dini wana mchango muhimu katika kuwahamasisha wananchi kusajili vifo ili taifa liwe na takwimu sahihi ya vifo vya wananchi wake.
Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza alipokuwa akifungua kikao cha hamasa kwa viongozi wa mkoa kuhusu majaribio ya mpango wa usajili wa vifo katika ukumbi wa mikutano wa Siasa ni Kilimo.
Masenza alisema kuwa viongozi wa dini ni nguzo muhimu katika utekelezaji wa mipango ya serikali kwenye maeneo yao. “Viongozi wa dini, naamini kabisa nyie ni nguzo muhimu katika kufanikisha usajili huu kwa sababu mnayo nafasi ya kukutana na wananchi wengi kila wiki, hivyo nawaomba tuwafikishie ujumbe huu. Naelewa fika mnayo namna ya kuwaeleza wananchi suala hili na likagusa mioyo yao” alisema Masenza. Aidha, aliwaomba viongozi hao wa dini, kupeleka taarifa za ujio wa zoezi hilo katika kila nyumba ya ibada na kuwahimiza viongozi walio chini yao kuendelea kurudia kuwakumbusha wananchi.
Aliwataka viongozi wa dini wanaposhirikishwa katika maziko ya waumini, wawakumbushe ndugu wa marehemu kusajili matukio hilo.
Majaribio ya maboresho ya mfumo wa usajili wa vifo yanafanyika kwa mara ya kwanza katika Mkoa wa Iringa kutokana na mkoa huo kufanya vizuri katika zoezi la usajili watoto wenye umri chini ya miaka mitano na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa.
=30=
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.