Dr,Robert Salim ,Mganga Mkuu wa Mkoa Iringa,leo amefungua semina ya kuelimisha Wanahabari kuhusu kampeni sirikishi ya chanjo dhidi ya surua,rubela na ugonjwa wa polio.
Amesema kuwa kampeni hii ni muhimu sana kwa Wanahabari kujua kwa kina juu ya kampeni ya ugonjwa huu ili kuleta uelewa kwa jamii,kwa sababu Wanahabari wanamchango mkubwa sana wa kuelimisha jamii na ujumbe utafika haraka na kwa wakati pasipo shaka kwa jamii.
Jukumu kubwa la Wanahabari ni kuwajulisha jamii juu ya faida na madhara ya ugonjwa huu wa surua,rubella na polio.Na pia wanao jukumu la kuondoa uvumi wowote kwa jamii maana wapo wananchi wanaopotosha juu ya chanjo hizo.
Chanjo hizi ni salama zimethibitishwa na shirika la Afya ulimwenguni na Wizara ya Afya,pia chanjo hizi utolewa bure kabisa.
Akifafanua Mratibu wa chanjo Mkoa Bw.Mwalongo ,amesema chanjo ya surua,rubela hutolewa miezi 9-59,na Polio utolewa miezi 18-42 na hadi mwaka 01 na nusu hadi 03 na nusu.
Kampeni hiyo itazinduliwa kesho na Mhe,Ally Hapi ,Mkuu wa Mkoa wa Iringa,katika kata ya NZIHI.Itafanyika kwa muda wa siku5,kuanzia tarehe 17/10 hadi 21/10/2019.Na Serikali imejipanga na chanjo zimekwishafika pamoja na vifaa tiba.
Daktari,Salim Amewaomba akina mama wawapeleke watoto wote ili wakapate chanjo hizo kwa muda muhafaka
Imetolewa na Humpphrey Kisika
Afisa Habari wa Mkoa wa Iringa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.