Naibu Waziri wa Maji Mhe. Mhandisi Marryprisca Mahundi amewataka wananchi kuendelea kuiamini Serikali ya awamu ya sita kutokana na kuendelea kutatua changamoto zinazowakumba wananchi hao ikiwemo suala la maji.
Ameyasema hayo wakati akiwa na kamati ya kudumu ya Bunge maji na Mazingira ilipotembelea katika kijiji cha Itagutwa kwaajili ya kukagua mradi wa maji wenye thamani ya shilingi Millioni 322 ambao utawanufaisha Zaidi ya Wananchi elfu moja miatano.
Akizungumza na Wananchi hao Mhe. Mahundi amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita inaaendelea kutekeleza ilani na kampeni ya kumtua mama ndoo kichwani hivyo kupitia mradi huo wa maji utaondosha changamoto ya maji katika kijiji hicho na vijiji jirani.
Pia ameongeza kwa kusema kuwa uwepo wa mradi huo waananchi watanufaika kwa kutotembea umbali mrefu kutafuta maji jambo ambalo linapelekea familia nyingi kuimalika kiafya na kiuchumi
Nae Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini RUWASA Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Mhandisi Exaud Humbo amesema kuwa mradi huo mpaka sasa wananchi watapata huduma ya maji kwa Zaidi ya asilimia 82.
Nao baadhi ya wananchi wameishukuru serikali kwa kuwaletea mradi huo ambao wamesema utazidi kuimarisha na kujenga familia kwani hapo awali walikuwa wakitembea umbali mrefu kutafuta maji jambo ambalo limepelekea ndoa nyingi kuvunjika.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.