Watendaji wa Serikali Mkoani Iringa wametakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kutekeleza Ilani ya uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza katika kikao cha tathimini ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi, Mnec wa CCM Mkoa wa Iringa Salim Abri (ASAS) amewataka kufanya kazi kwa bidii ili chama kisiendelee kubeba lawama na kujibia changamoto ambazo zilipaswa kujibiwa na watendaji wa Serikali.
"Niwaombe watendaji wa Serikali mfanye kazi kwa bidii ili mtupunguzie mzigo wa kujibia changamoto ambazo ninyi mlipaswa kujibu, mkifanya vibaya sisi viongozi wa Chama ndiyo tunaoanza kuwajibishwa na wananchi" amesema Salim
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.