Halmashauri za mikoa ya nyanda za juu kusini zimetakiwa kutenga maeneo maalum kwa ajili ya wajasiriamali kutekeleza majukumu yao.
Kauli hiyo ilitolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu alipotembelea mabanda ya maonesho ya Halmashuri ya Mji Makambako na Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo katika uwanja wa Nanenane mjini Mbeya.
Ayubu alisema kuwa wasindikaji katika Halmashauri wasiachwe kufanya kazi za kusindika bidhaa majumbani. “Wasindikaji wameshuhudia kuwa wanafanya kazi za usindikaji nyumbani badala ya kufanya kazi hizo katika maeneo rasmi. Serikali ilikwisha zielekeza mamlaka za serikali za mitaa kutenga maeneo kwa ajili ya wajasiriamali kuweza kutekeleza majukumu yao. Maeneo hayo lazima yawe yenye miundombinu ya maji na umeme na kufikika kwa urahisi” alisisitiza Ayubu. Aidha, aliongeza kuwa Halmashauri ziwasaidie wajasiriamali kufikia viwango vya ubora unaotakiwa na kuwasaidia kupata nembo ya ubora ya TBS na ‘Barcode’ ili kuweza kupata soko la ndani na nje ya nchi.
Maonesho ya shughuli za wakulima Nanenane mwaka 2017 yanaongozwa na kaulimbiu isemayo, “zalisha kwa tija mazao na bidhaa za kilimo, mifugo na uvuvi kufikia uchumi wa kati”.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.