Mhe Mkuu wa Mkoa wa Iringa Halima Dendego, amepokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mhe Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Fatma Mwasa Leo hii katika kata ya Mapanda. Mwenge wa Uhuru umekagua na kuweke mawe ya msingi katika miradi 5 iliyotekelezwa na Halmashauri ya Mufindi.
Mhe Rc Dendego akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mhe Saad Mtambule Mkuu wa Wilaya ya Mufindi amewata kuhakikisha wanapokea ushauri na maelekezo yote yatakayo tolewa na Mkimbizi Mwenge Ki Taifa ndugu Galaluma. Mhe DC Mtambule, akitoa salamu za Wilaya ya Mufindi amesema Mwenge wa Uhuru utakagua miradi yenye thamani ya zaidi ya milioni 900. Ndugu, Galaluma amepongeza Uongozi wa wa Wilaya ya Mufindi na wananchi kwa kujipanga kuupokea Mwenge wa Uhuru na kutekeleza miradi kwa kuzingatia thamani ya fedha.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.