Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, IRINGA
Kamati ya maandalizi ya kampeni ya Furaha yangu Mkoa wa Iringa imetakiwa kuweka mikakati kwa ajili ya kufanikisha kampeni hiyo kwa kuwafikia wananchi wengi zaidi.
Kauli hiyo ilitolewa na mwenyekiti wa kamati kuu ya maandalizi ya kampeni ya Furaha yangu mkoa wa Iringa, Dkt. Robert Salim alipokuwa akifungua kikao hicho katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa leo.
Dkt. Salim ambaye pia ni mganga mkuu wa Mkoa wa Iringa alisema kuwa dhamira ya mkuu wa Mkoa ni kuona kampeni hiyo inafanikiwa katika Mkoa wa Iringa. Alisema kuwa mafanikio hayo yatatokana na ushirikiano baina ya serikali na wadau mbalimbali wa mapambano ya VVU na UKIMWI mkoani Iringa. Aliwataka wajumbe hao kuweka mikakatik itakayowezesha wananchi wengi kufikiwa na kampeni hiyo ya Furaha yangu.
Kampeni ya “Furaha Yangu” inaonesha dhamira ya Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais, Dkt. John Magufuli kuongeza kasi ya mapambano ya VVU na UKIMWI katika kuzifikia “tisini tatu” na mwelekeo kuwa wa kufikia “sifuri tatu”; kutokuwepo kwa maambukizi mapya ya VVU, kutokuwepo kwa unyanyapaa kwa watu wanaoishi na VVU, na kutokuwepo na vifo vinavyotokana na UKIMWI ifikapo mwaka 2030.
Kampeni ya Furaha yangu mkoani Iringa itazinduliwa tarehe 24 Julai, 2018 katika uwanja wa Kichangani mjini Iringa na mkuu wa mkoa wa Iringa, mhe Amina Masenza.
=30=
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.