Leo February17,2023 Kamati ya siasa ya chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Iringa imeendelea na ziara ya kukagua utelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020-2025 katika halmashauri ya wilaya ya kilolo ambapo licha ya kuridhishwa na kazi nzuri ya usimamizi wa miradi ya Maendeleo katika sekta ya elimu,Afya,Maji,kilimo na Umeme imetuagiza sisi kama watumishi kuendelea kutekeleza majukumu yetu kwa kuzingatia masilahi mapana ya wananchi ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye amejipambanua kuwatumika watanzania kwa kazi zake anazo zifanya.
Nitumie nafasi hii kuwapongeza wajumbe wa kamati ya siasa ya chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Iringa kwa kazi nzuri ya usimamizi wa Ilani ya chama na sisi kama watumishi tutaendelea kufanya kazi kwa vitendo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.