Msanii na Balozi wa kampeni ya Mtu ni Afya iliyopo chini ya wizara ya Afya Ndg. Mrisho Mpoto amewataka wananchi wa kata ya Migoli iliyopo Halmashauri ya Iringa kukabiliana na Swala la udumavu Kwa kuhakikisha kila familia inakula vyakula vyenye lishe Bora.
Ameyasema hayo septemba 02, 2024 wakati wa Kampeni ya Mtu ni Afya iliyofanyika eneo la Migoli ikiwa Ni mwendelezo wa Kampeni ya Mtu ni Afya inayohusisha Afua tisa ikiwemo Usafi wa mazingira.
Aidha Ndg. Mrisho Mpoto ameongeza kuwa watoto Kwanzia mwaka sifiri na kuendelea wanapaswa kupewa lishe Bora ili kuwajenga akili na kutokomeza tatizo la udumavu, licha ya hayo ameongeza kuwa wazazi wanapaswa kujali wanachomlisha mtoto kwani kujaza tumbo siyo lishe Bora.
Kampeni hiyo ya mtu ni Afya kitaifa ilizinduliwa Mei 9, 2024 Mkoa wa Pwani ambapo kwa Mkoa wa Iringa ilizinduliwa Agosti 21,2024 ikiwa na lengo la kuhakikisha wananchi wanafanya kweli kwenye swala zima la usafi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.