Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Daniel Chongolo amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Iringa Halima Dendego kuhakikisha mpaka kufikia Julai Mosi mwaka huu kituo cha afya cha Banda Bichi kiwe kimefunguliwa na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.
Aidha Chongolo amesema kufikia Julai Mosi atahakikisha Halmashauri ya Wilaya ya Iringa inakabidhiwa gari tatu ,mbili za kubeba wagonjwa na moja ya kufatilia shughuli mbalimbali ikiwemo ukaguzi.
Ametoa agizo hilo Mei 29,2023 alipokuwa akizungumza na wananchi baada ya kushiriki Mkutano Kwa Balozi wa Shina Na. 04 Kata ya Ifunda katika halmashauri ya wilaya ya Iringa, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku saba ya kukagua uhai wa chama na utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025.
Amesema haiwezekani Serikali ijenge majengo mazuri na yenye vifaa vya kisasa lakini hakuna huduma zinazotolewa kwa wananchi kitu ambacho hawezi kukubaliana nacho kama mtendaji mkuu wa chama.
Aidha Chongolo amemuagiza Meneja wa Mamlaka ya Maji Safi na Mazingira vijijini Joyce Bahati kuhakikisha mpaka kifikia desemba 31,2023 maji safi na salama katika kata ya ifunda yanatoka ili wananchi wasiendelee kuhangaika kufata maji mwendo mrefu.
Katibu wa Nec Oganaizesheni wa Chama cha Mapinduzi Issa haji Gavu amewataka wanachama wa CCM kuhudhuria vikao sambamba na kulipia kadi ili waendelee kuwa wanachama hai.
Gavu amesema hayo Mei 29,2023 alipokuwa akizungumza na wananchi baada ya kushiriki Mkutano Kwa Balozi wa Shina Na. 04 Kata ya Ifunda katika halmashauri ya wilaya ya Iringa akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa CCM ambaye yupo mkoani Iringa kwa ziara ya siku 7 ya kukagua uhai wa chama na utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM.
Amesema kuwa wanachama hai itasaidia CCM kuendelea kuwa chenye mvuto na oitaendelea kuaminiwa na kuthaminiwa na watanzania huku akisema hakuna chama chenye mvuto kwa wananchi kama CCM.
Katika hatua nyingine GAVU amesema Tanzania ni nchi yenye demokrasia ndio maana kumekuwa na majadiliano sambamba na kumpa Uhuru kila mtanzania kutoa maoni.
Katibu wa Nec Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi Sophia Mjema mfumo wa M-Mama ambao umeanzishwa hapa nchini umesaidia kupunguza vifo vya akina Mama wajawazito wanapotaka kujifungua.
Mjema amesema hayo Mei 29,2023 alipokuwa akizungumza na wananchi baada ya kushiriki Mkutano Kwa Balozi wa Shina Na. 04 Kata ya Ifunda katika halmashauri ya wilaya ya Iringa akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa CCM ambaye yupo mkoani Iringa kwa ziara ya siku 7 ya kukagua uhai wa chama na utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM.
Amesema Mkoa wa Iringa ni miongoni mwa mikoa ambayo mwaka huu 2023 wanatarajia kuanza kuanza kwa mradi huo wa M- Mama ambapo utakwenda kusaidia wanawake wengi wajawazito ili wasipoteze maisha wakati wa kujifungua.
Amewakumbusha wananchi wa Ifunda kuendelea kujikinga na maambukizi ya Virusi vya ukimwi kwa kuwa mkoa wa Iringa takwimu zinaonyesha maambukizi yapo juu.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Daniel Chongolo amemuagiza Waziri wa Kilimo Bashe kwenda katika kata ya Masaka ndani ya wiki tatu akiwa na wataalam wake kuangalia namna ya kujenga skimu ya umwagiliaji kwa kuwa maji yako.
Chongolo amesema hayo Mei 29, 2023 muda mfupi baada ya kuzindua upandaji wa samaki katika mradi wa Bwawal la Masaka, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku 7 Mkoani Iringa.
Amesema fedha ikitiengwa kwa ajili ya akimu hiyo ya umwagiliaji na kuweka miundombinu ili skimu ianze kufanyakazi.
Chongolo amempongeza Waziri wa Maji Juma Aweso kwa kazi kubwa anayofanya kwa kupeleka bwawa hilo la masaka huku akitaka kutengwa bajeti zaidi ili kujengwa mabwawa mengi zaidi yatakayoleta matokeo chanya.
Aidha Chongolo ameitaka halmashauri ya wilaya ya Iringa kuhakikisha wanaendelea kutunza mazingira ili maeneo hayo yawe kivutio huku akiwataka halmashauri kupanda miti ya matunda ili iwe sehemu ya utalii.
Amewaomba watanzania kuendelea kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha anapeleka maendeleo katika kila kona ya nchi .
Awali Afisa Uvuvi wilaya ya Iringa Kelvin Ndege amemweleza Katibu wa CCM Chongolo kuwa Bwawa la Kisaka lina ukubwa wa kilomita za mraba 5.33 huku bwawa hilo litawanufaisha wananchi zaidi ya elfu-10 ndani na nje ya kata ya Masaka.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.