Kikao hicho ambacho kimefanyika leo tarehe 06/12/2019 Mkoa Mkoani humo. Iringa ni kati ya Mikoa iliyofanya vizuri katika mitihani ya Darasa la Saba kwa mwaka 2019 kati ya Mikoa 26 ya Tanzania Bara. Mkoa wa Iringa umekuwa katika nafasi ya tatu ngazi ya Taifa na kupata tuzo bora ya ufaulu.
‘Nawapongeza walimu na watendaji wote kwa kufanya vizuri katika usimamizi wa mitihani ya Darasa la Saba kwa mwaka huu 2019 na kupata nafasi hii ya tatu Kitaifa’. Ameyasema haya wakati wa kikao hicho Katibu Tawala wa Mkoa Bi. Happiness Seneda ambaye ndiye alikuwa Mwenyekiti wa kikao hicho.
Wanafunzi 25,325 walisajiliwa katika shule 496, sawa na 98.7% walifanya mitihani hiyo. Na 88.53% wamefaulu mitihani hiyo, ambapo ni ongezeko la 5.0% la 88.53% ukilinganisha na mwaka 2018 ambapo ilikuwa 83.06%.
Nawapongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo kwa kuongeza ufaulu kwa 7.82% tofauti na mwaka jana. Ufaulu ni jambo muhimu sana kwetu, japo kuna changamoto za vyumba vya madarasa. Jumla ya watoto 3,480 hawajapangiwa kuanza kidato cha kwanza kutokana na ukosefu wa nyumba vya madarasa.
Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo zihakikishe wanashughulikia miundombinu ya vyumba vya madarasa ili watoto waanze shule mwezi Januari. Nawapongeza Halmashauri ya Mji Mafinga na Halmashauri ya Wilaya ya Mifindi kwa kutokuwa na upungufu wa vyumba vya madarasa.
Mwaka huu 2019 Mkoa haukukumbwa na tuhuma za udanganyifu, nawapongeza sana Kamati ya Mitihani kwa kusimamia vizuri.
Wito wang naomba usimamizi huu uendelee hadi ngazi ya Taifa.
Matokeo:
Waliofanya mtihani ni 24,784 (Wavulana 11,421 Wasichana 13,363), Waliofaulu kuanzia 100 – 250 ni 20,606 (Wavulana 9,513 Wasichana 11,093) sawa na 88.53% ukilinganisha na mwaka 2018 ambapo ilikuwa 83.4%, hivyo kwa mwaka huu 2019 matokeo yamepanda kwa 5.3%.
Imetolewa na Ofisi ya Habari Mkoa,
Humphrey Kisika.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.