Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa Bi. Doris Kalasa ametembelea na kukagua vituo vya kujiandikishia wapiga kura huku akiwataka waandikisha kuwa wakarimu pindi wanapowahudumia wananchi.
Bi. Kalasa ameyasema hayo leo Octoba,10,2024 akiwa ameongozana na mratibu wa uchaguzi Mkoa wa Iringa Bi. Nuru Sovellah pamoja na Katibu Tawala wa Wilaya ya Iringa Ndg. Michael Semindu wakati akikagua vituo vya kujiandikishia katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.
Bi. Kalasa amesema kuwa ili zoezi hilo liweze kufanikiwa kwa asilimia 100 kwanza kabisa kuhamasisha watu kwa wingi lakini pili wananchi wanapofika katika vituo hivyo waandikishaji waweze kuwa na mapokezi mazuri kwa wananchi jambo ambalo litapelekea wananchi kushawishika na kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la Orodha ya Wapiga kura katika uchaguzi wa Serikali za mitaa.
Pia Mhe. Kalasa amewahimiza waandikishaji hao kujali sana suala la muda wa kutoa huduma huku akiwataka kuwahi kufika katika vituo hivyo kama muda ulivyopangwa na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.
Zoezi la uandikishaji katika Daftari la Orodha ya Wapiga kura linatarajiwa kuzinduliwa na kuanza kesho Octoba 11,2024 hadi Octoba,20,2024
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.