Mkuu wa mkoa wa İringa Mhe. Halima O. Dendego ameendelea kuongoza mjadala wa kitaifa wa Nishati Safi ya Kupikia uliofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo ulioudhauriwa na viongozi na wadau mbalimbali.
Katika mjadala huo mada mbalimbali zimejadiliwa ikiwa ni pamoja na Sera, Sheria, Kanuni na Mifumo ya Udhibiti ya Kuwezesha Nishati Safi ya Kupikia, Teknolojia na Ubunifu Katika Nishati Safi ya Kupikia, Fursa za Ajira na Ujuzi Unaohitajika Katika Mabadiliko ya Kutumia Nishati Safi ya Kupikia, Kuhamasisha Wanawake Kuchukua Hatua za Kutumia Nishati Safi ya Kupikia pamoja na Mafunzo na Uzoefu Kutoka kwa Wengine.
Akifunga Mjadala huo Mhe. Dendego amesema kuwa mpaka sasa mkoa wa Iringa tayari una wadau ambao wamekwisha anza kazi na wao kama Mkoa wapo tayari kuhakikisha wanatoa Elimu na kuwahamasisha juu ya Nishati Safi ya Kupikia.
Imetolewa na Afisa Habari Mkoa wa Iringa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.