Ikiwa ni kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo hufanyika March 08, kila Mwaka Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego ameitumia siku hiyo kuzindua kampeni endelevu ya Kukabiliana na Udumavu kwa watoto na kumtua mama Kuni kichwani.
Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo Mhe. Dendego amesema kuwa Mkoa umetumia siku ya wanawake kuzindua mkakati wa kukabiliana na udumavu wa watoto ambao utawafikia wananchi wote kuanzia mjini hadi vijijini.
Pia Mhe. Dendego amewataka wanawake kumuunga Mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuanzisha kampeni ya matumizi ya nishati safi ili kunusuru misitu na kulinda afya zao, katika hafla hiyo Umoja wa wanawake Mkoani Iringa UWT kwa kushirikiana na wadau walitoa zawadi ya mitungi ya gesi kwa Mamia ya wanawake wa Iringa
Nao baadhi ya Wanawake wa Mkoa wa Iringa wameishukuru Serikali kwa kuwapa mitungi hiyo na kumshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuanzisha kampeni hiyo huku wakiiomba Serikali kupunguza gharama za nishati safi kama gesi na mkaa mbadala ili kila mwananchi aweze kuzimudu na kuachana kabisa na matumizi ya nishati ya mkaa na kuni.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.