Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba amewataka Madiwani Mkoani Iringa kuhakikisha wanaisimamia miradi yote iliyopo kwenye kata zaoAmeyasema hayo leo Mei,28,2024 wakati aliposhiriki katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa lililofanyika kwenye ukumbi wa Siasa ni Kilimo.Akizungumza na Wah. Madiwani hao Mhe. Serukamba amesema kuwa miradi mingi kwenye Halmashauri bado haijakamilika na hii ni kutokana na kukosekana kwa usimamizi wa miradi hiyo, hivyo amewataka madiwani kuhakikisha wanasimamia kwa nguvu zao zote miradi hiyo na kuachana na visingizio vya kusema kuwa wataalamu ndio wanaopaswa kusimamia miradi hiyo."Mkurugenzi madiwani wote hawa ni wa kwako, wote watume wakasimamie kazi za miradi iishe kwa wakati,ndugu madiwani hakikisheni mnasimamia miradi iishe kwa wakati"Pia Mhe. Serukamba ameongeza kwa kutoa rai kwa uongozi wa Halmashauri hiyo kuhakikisha pindi fedha za miradi zinapofika ziende moja kwa moja kwenye miradi na zisikae Halmashauri ili miradi iweze kukamilika kwa wakati.Kwa upande mwingine Mhe. Serukamba ameendelea kuwahimiza madiwani katika Halmashauri hiyo kuwa na umoja na mshikamano katika kuisongesha mbele Halmashauri hiyo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.