Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdullah amewataka wakufunzi wa sensa ya watu na makazi kuzingatia mafunzo waliyoyapata na kutanguliza mbele misingi ya uzalendo katika kutekeleza majukumu yao ili kufanikisha malengo mahususi ya kidemografia ambayo ni muhimu kwa ustawi wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdullah amesema hayo wakati akifunga mafunzo ya wakufunzi wa sensa ya watu na makazi kitaifa mkoani Iringa ambapo amesema sensa ya watu na makazi 2022 inatarajiwa kuwa na matokeo chanya kufuatia maandalizi mazuri na matumizi ya vifaa vya kidigitali.
Aidha Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Queen Sendiga amemuhakikishia Mhe. Hemed Suleiman kuwa kama mkoa wa Iringa wamejipanga vizuri kutekeleza zoezi la sensa na kwa umakini zaidi.
Naye Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Idadi ya Watu (UNFPA), Dk. Wilfred Ochan amesema ameridhishwa na utayari ulioonyeshwa na Serikali ya awamu ya 6 ktk kutekeleza jukumu muhimu la kufanya sensa ya watu na makazi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.