Mkuu wa Mkoa Mheshimiwa Ally Hapi Aongoza Mkutano wa Baraza la Madiwani Kujadili Hoja za Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Tarehe 15 Mei, 2020
Pamoja na salamu mbalimbali Mheshimiwa Hapi ametumia fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu na kupata nafasi katika mkutano huu kujadili hoja za Mkaguzi wa Serikali kwa mwaka unaoshia 2018/2019. Pia Mheshimiwa Hapi amewapongeza kwa kupata hati safi, hii imekuwa kwa miaka mitatu mfululizo, na kuongeza kuwa kupongeza Halmashauiri zote tano za Mkoa wa Iringa kwa kufanya vizuri.
Amesema kuwa, mafanikio haya yanatokana na ushirikianokwa Madiwani, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Wakuu wa Idara na watendaji wote katika Halmashauri, na kusema kuwa hoja zote ambazo hazijafungwa zitajadiliwa vizuri na kufunga.
Mheshimiwa Hapi ametoa rai kwa watendaji wa Halmashauri hiyo kuwa:
-Kuhakikisha hoja za mwaka 2018/2019 na za miaka ya nyuma zinafanyiwa kazi.
-Kukusanya madeni kiasi cha Tsh. Bilioni 1.6 ambazo zinaonekana zimekusanywa lakini hazijawasilishwa.
-Halmashauri pia ihakikishe kiasi cha Tsh. 2.1 bilioni wanazodai watu mbalimbali kama wakandarasi, stahiki za watumishi zilipwe kwa wakati. Aidha katika taarifa ya CAG kiasi cha Tsh. 1.1 bilioni zinadaiwa, hivyo kuonesha Halmashauri haijishughulishi na madeni ya watoa huduma.
-Halmashauri isimamie mali zake, inaonesha kuna magari mawili ni mabovu hayatembei.
-Kuhakikisha Halmashauri inatenga 10% ya mapato ya ndani kwa ajili ya mikopo kwa walemavu, vijana na wanawake. Inaonekana katika kiasi cha Tsh. 125 milioni ilishindwa kuchangia.
-Fedha zilizopo kwenye akaunti ya Amana zitumike kwa makusuidi yaliyokusudiwa.
-Halmashauri ihakikishe inapata wakandarasi wenye sifa katika miradi ya maendeleo
Mheshimiwa Hapi pia ametumia fursa hii kuwaambia Halmashauri kuwa, sababu kubwa ya kuwepo kwa hoja hizi ni kutokana na kutokuwa makini katika mifumo bora ya kukusanya mapato.
Pia Mheshimiwa Hapi ameendelea kuwaasa wananchi kuchukua tahadhali juu ya janga la ugonjwa Covid-19, kwani weninge wanasema kuwa ugonjwa haupo, ila nawaambia tu kuwa ugonjwa huu upo sana tu, na tuendelee kuchukua tahadhali. Amesema kuwa, Mkoa wetu upo barabarani na kuunganisha mikoa mingine na nchi za jirani, hivyo tunapata wageni wengi mbalimbali wanaopita katika Mkoa wetu.
Uwamuzi wa Serikali wa kuruhusu shughuli za kiuchumi ziendelee na jambo jema kwetu, kwani tungefunga uchumi sasa hivi tungekuwa tunahali mbaya ya kiuchumi, kwani sisi ni nchi inayoendelea. Naomba tushikamane na tuchukue tahadhali.
Kwa sasa tunaelekea mwishoni mwa uhai wa Baraza na kuelekea kwenye uchaguzi, nawashukuru sana, kwani tumefanikisha mambo makubw ya kimaendeleo. Namshukuru kipekee Mheshimiwa Mhapa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kwa kushirikiana nami kama Mkuu wa Mkoa wa Iringa katika shughuli zote za maendeleo kwa kipindi chako chote ulichokuwa madarakani.
Maagizo kwa Halmashauri:-
-Kuwepo kwa malalamiko ya watumishi waliopandishwa vyeo na madaraja kutoshughulikia stahiki zao
-Upatikanaji wa maji safi na salama
-Mikopo kutolewa kwenye vikundi vilevile tu bila kujali kama kuna vikundi vingine. Kuna vikundi vya Upendo na Mshikamani vya Kata ya Nyang’oro havijawahi kupata mikopo.
-TARURA kushughulikia barabara zote zilizoharibiwa na mvua
Mheshimiwa Hapi alimaliza kwa kusema, nawatakia uchaguzi mwema kwa wagombea watarajiwa wote.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.