Mhe.Asia Abdalah (DC Kilolo) wa pili toka kushoto,akiwaamemwakilisha Mhe,Mkuu wa mkoa wa Iringa,katika kilele cha maenesho ya Nanenane yaliyofanyika jijini Mbeya.Mgeni rasmi wa maonesho hayo alikuwa Mhe,Peter Pinda(Waziri Mkuu Mstaafu).Katika maonesho hayo ambayo imeshiriki mikoa 7 ya Nyanda za juu kusini,Mhe.Pinda,alitembea mabanda kadha kwa mujibu wa ratiba ili kujionea shughuli wanazofanya na mazao walizonazo,katika mkoa wa Iringa tulipata bahati ya kutembelewa Halmashauri ikuiwemo Halmashauri ya wilaya ya Mufindi na Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo.Mgeni rasmi alifurahishwa sana alipoona wakulima,na wafugaji wanavyopambana na kijikwamua na wimbi la umaskini na kuwataka kuendelea kutoa Elimu ya kilimo,Uvuvi na ufugaji kwani itasaidia kwa wananchi mmoja mmoja kufikia uchumi wa kati.Katika hotuba yake Mhe.Pinda,ameagiza mikoa 7 ya Nyanda za juu kusini ihakikishe ipambane kwa kuzalisha chakula kwa wingi na kutokomeza UTAPIA MLO ambao umekuwa ni tatizo kwa mikoa hii 7.Pili ameagiza viongozi wote wahakikishe vijana wanashirikishwa kikamilifu katika shughuli za uzalishaji mali ili kuleta maendeleo katika Taifa.Katika kilele cha maonesho ya Nanenane 2019 Mhe,Pinda alikabidhi zawadi kwa wakulima na wafugaji waliofanya vizuri,ambapo Halmashauri ya Kilolo,ilipata zawadi ya Mfugaji bora kikanda na Halmashari ya Wilaya ya Iringa ilishinda nafasi ya pili kikanda kwenye eneo la kilimo,walikabidhiwa kombe na cheti.Tunatoa hongera kwa Halmashauri zote kwa kushiriki vyema pamoja na wakulima,wafugaji na sekta ya uvuvi kwa ushindi huo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.