Mapema Leo hii Julai 17, 2023 Mkuu wa Mkoa Iringa Mhe Halima O. Dendego ameongoza kikao Maalumu cha kujadili Mchakato wa Maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Siasa ni Kilimo ulipo Mkoa wa Iringa.
Mjadala huu umehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali, Viongozi wa vyama vya Siasa, Wataalamu kutoka Vyuo Vikuu, Wadau wa Maendeleo, Sekta binafsi, Viongozi wa dini pamoja na makundi mbalimbali katika Jamii.
Hakika Dira hii inatarajiwa kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi na kijamii ili kufikia lengo la kuwa Taifa lenye ustawi kwani dhamira ya Serikali yetu ni kuhakikisha katika maandalizi ya Dira hii Watanzania wote kutoka matabaka mbalimbali ya maisha, makundi mbalimbali yanapata nafasi ya kuchangia mawazo yao.
"Mchakato wa maandalizi ya Dira ya 2050 Sekretarieti na wadau wengine watatumia vyombo vya habari ikiwamo mitandao ya kijamii ili tupate maoni kuhusu dira mpya hivyo wadau wote tushiriki kutoa mchango utakaowezesha kuandaliwa kwa Dira mpya yenye maono ya watanzania kwa miaka 25 ijayo"
Aidha tunaishukuru na kuipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutekeleza Mpango wa miaka 25 ya Maendeleo na sisi Mkoa wa Iringa tunajivunia mafanikio hayo.
Imetolewa na Afisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.