Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego akiwa ameambatana na viongozi wa Mbalimbali wa Mkoa wakiwemo Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, viongozi wa Chama cha Mapinduzi na Kamati ya ulinzi na Usalama Mkoa wa Iringa wametoa Mkono wa pole kwa Waathirika wa Mafuriko Wilaya ya Hanang Mkoa wa Manyara
Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Mkoa wa Iringa Mhe. Dendego ametoa salamu za pole kwa waathirika wote na kwa wale wote walioondokewa na ndugu, jamaa na marafiki na kuwataka Watanzania kuendelea kujitokeza kuendelea kutoa misaada katika eneo hilo
Nae mkuu wa Wilaya ya Hanang Mhe. Janeth Mayanja ametoa shukrani nyingi sana kwa Serikali kwa kuwa karibu nao katika nyakati zote pia kwa Wananchi wa Mkoa wa Iringa na Watanzania kwa ujumla kwa Moyo wao wa upendo kwani toka tukio hilo lilipotokea ni watu wengi wamejitokeza kwa kutoa pole na kutoa misaada
Wakiwa katika wilaya hiyo wametembelea katika maeneo yaliyoathiriwa na kujionea hali ilivyo kwa sasa huku wakipongeza kazi kubwa inayoendelea kufanywa na Serikali kwa kushirikiana na wananchi katika kuhakikisha hali inakuwa shwari kama hapo awali
Msaada uliotolewa na Mkoa wa Iringa ni chumvi, mahindi,ndoo za maji,mchele,mashuka, unga, magodoro, mkaa mweupe na milunda ya miti ambapo msaada huu una thamani ya jumla Shillingi . 42,944,000.00
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.