Mheshimiwa Hapi ameyasema hayo katika semina iliyoandaliwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) iliyofanyika Mjini Mafinga Februari 10, 2020.
Akifungua semina hiyo Mheshimiwa Hapi amesema, ‘mtakumbuka tulikuwa na mashirika mengi sana ya Hifadhi ya Jamii ikiwemo LAPF, NPF, EGPF nk, lakini SErikali imeamua kuunganisha mashirika hayo na kuwa mfuko mmoja ambao utahudumia wafanyakazi wa Serikali ambao kwa sasa baada ya kuunganishwa unaitwa PSSSF, na NSSF imebaki kuhudumia wafanyakazi wa Sekta Binafsi. Sheria hii inamtaka Mwajiri kupeleka michango ya mwanachama kila mwisho wa mwezi bila kukosa na bila kuchelewesha. Kwani baadhi ya Waajiri wamekuwa wakichelewesha michango ya wanachama, lakini sasa Serikali imeweka sheria kali kuwa, Mwajiri akichelewesha michango atapata faini, na asipopeleka kabisa basi atapata penati.
Ameongeza kuwa, Sekta zisizo rasmi kama bodaboda, Mama Nitilie, na wajasiriamali wengine wadogo wadogo wanatakiwa kuwa wanachama wa mfuko ili kujiwekea akiba. Hii itasaidia kuwainua wafabiashara/wajasiriamali katika kukuza uchumi, kwani sekta hii isiyo rasmi ina mchango mkubwa sana katika Taifa.
Tanzania imeingia katika ubora wa mazingira mazuri ya uwekezaji kwa wajariamali wadogo, tumekuwa nchi ya 21 duniani katika ubora huo ikiongozwa na India ikifuatiwa na China. Hivyo tuna nafasi kubwa sana ya kuwaendeleza wajasiriamali hawa ili kukuza uchumi wa Taifa. Katika Mkoa huu tumetoa vitambulisho 60,000 kwa wajasiriamali na tumepata zaidi ya bilioni 1, itakuwaje kwa Tanzania nzima?
Wito kwa NSSF, ni muhimu kuwafikia wajasiriamali wote 60,000 wa mkoa huu, pia mnawaelekeza faida za mfuko kama matibabu, mikoo baada ya kustaafu, mafao ya uzazi nk.
Pia ameongeza kwa Waajiri kuwa, hakikisheni michango inaenda kwenye mifuko kwa wakati, watu wanaostaafu wapate mafao yao kwa wakati, tena mjivunie wastaafu, kwani mkiwalipa kwa wakati wataipatia sifa njema mfuko. Hii itasaidia kuokoa wastaafu kukopa fedha katika mashirika yenye riba kubwa (fedha za moto). Waajiri wahakikishe watumishi wote wamejiandikisha kwenye mfuko.
Pamoja na semina ya NSSF, Mheshimiwa Hapi amepata nafasi ya kukabidhi majengo yaliyokuwa yanatumika na Kampuni ya Wachina ya kutengeneza barabara, na kuwa Kituo cha Afya cha Changarawe Mjini Mafinga. Majengo hayo yenye ofisi na nyumba 8 za watumishi yatasaidia kuondoa msongamano wa wagonjwa katika Hospitali ya Mji Mafinga.
Pia ametembelea mradi wa ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Mufindi na kujionea ujenzi unaondelea. Japo kuna mapungufu katika umaliziaji ambao unatokana na ucheleweshwaji wa vifaa Mheshimiwa Hapi ametoa siku kumi na nne kukamilisha ujenzi huo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.