Mhe Qeen Sendiga Ameyasema hayo leo juni 21 kwenye ufunguzi wa warsha ya kuwajengea uwezo wa wawezeshaji wa vituo vya mradi wa SEQUIP yenye jukumu la kuboresha ubora wa elimu kwa wanawake ambao tayari wamejifungua na wameamua kurujea tena shuleni,
amezungumza hayo alipokuwa katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu kreluu kwenye warsha hiyo na kuwasisitiza katika mda mfupi wa mafunzo hayo wakufunzi wa mradi wa SEQUIP kuhakikisha wanafwata kilicho waleta ili waende kuwa wakufunzi bora katika majukumu yao ili wawe mabalozi wazuri.
Mhe Mkuu wa Mkoa Sendiga, aliongeza kwa kuwataka wakufunzi kutoa upendo kwa wanafunzi wao japo wanafunzi wao ni wazazi tayari na kutotumia lugha zisizofaa katika majukumu yao na kukamilisha majukumu yao kwa upendo.
Mratibu wa SEQUIP Taifa Baraka Kionywaki amemweleza Mhe Sendiga kuwa moja ya jukumu walonalo wao kama SEQUIP ni kutoa elimu ya sekondari kwa njia ya mbadala, hata hivyo alimweleza kuwa mpaka sasa wamepokea bilioni 3 kutoka serikalini ili kutekeleza mradi huo ikiwa na kujenga majengo kwenye Mikoa tofauti ikiwemo na Iringa wameshajenga madarasa 4 jengo la kulelea watoto na jengo la utawala katika eneo la Mawelewele.
Baraka amesema kuwa Ki Taifa wapo wanafunzi 3333 ambao tayari wamesha sajiliwa na Mkoa wa Iringa umesha sajili wanafunzi 189, ambao kituo cha Saba Saba kuna wanafunzi 67 na 69 wako Chuo cha maendeleo ya jamii ipogoro, mafinga wapo 22 na Igowole wapo wanafunzi 30.
Hata hivyo mradi una walimu 802 Nchi nzima vituo vipo 131, na kati ya hivyo Mkoa wa Iringa una vituo 6.
Imetolewa na Afisa habari Mkoa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.