Mapema leo hii Mkuu wa mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego ameshuhudia zoezi la utiaji saini wa hati ya udhibiti wa wafanyabiashara holela ambapo amewataka wafanyabiashara wadogo wadogo (Machinga) kurudi katika sehemu zao kwa kufuata sheria zilizopo.
Akizungumza katika mkutano huo Mhe. Dendego amesema kuwa katika kipindi hiki kumeripotiwa kuwa na mvua nyingi hivyo sio vyema kuwakuta wafanyabiashara na machinga wakifanya biashara zao kwenye maeneo ambayo sio rasmi kama pembezoni mwa barabara,mitaroni na vichochoroni hivyo basi ifikapo tarehe 19/11/2023 watu wote waliopo katika maeneo yasiyo rasmi wawe wameondoka na kwenda kwenye maeneo waliopangiwa na Serikali.
Pia Dendego amesema kuwa kwa wale wote ambao wamekosa maeneo ya kufanyia biashara basi ni wakati sasa wa wao kuonana na uongozi wa Halmahsuri kuhakikisha wanapatiwa maeneo ya kufanyia biashara kwani kuanzia tarehe 20/11/2023 uongozi wa Mkoa, Wilaya na Halmashauri ya Manispaa wataanza oparesheni ya kufanya usafi katika Hlmashauri Manispaa ya Iringa.
Nao baadhi ya viongozi wa wafanyabiashara, machinga na viongozi wa masoko wameishukuru serikali ya Mkoa kwa zoezi na maamuzi waliyoyafanya ya kuhakikisha mji wa Iringa unapendeza na kuwa safi.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.