Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe.Peter Joseph Serukamba ameomba ushirikiano kutoka kwa wananchi wa Mkoa wa Iringa na kuahidi atashirikiana nao katika kufanya kazi na kutatua Changamoto mbalimbali zilizopo Mkoani Iringa.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya Ofisi kati yake na Mkuu wa Mkoa wa Singida, amesema kuwa hatokuwa mtu wa kukaa Ofisini bali atatoka na kwenda vijijini kutatua changamoto za wananchi.
"Mimi sio Mkuu wa Mkoa wa kukaa ofisini hivyo tutakwenda vijijini mimi na Wakuu wa Wilaya ili kufikia mwezi wa saba tuwe tumekifikia kila kijiji na tumebaini changamoto zao na kuona namna ya kuzitatua",
Mhe.Serukamba anahamia Iringa akitokea Mkoa wa Singida akibadilishana na Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego anayeenda Mkoani Singida.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.