Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Queen Sendiga amesema Nimepata Taarifa ya kuwepo na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya kilolo kuishi nje ya maeneo yao ya kazi ambapo amemtaka mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuwa chukulia hatua kali watumishi hao.
Nakuagiza mkurugenzi kuwa ifikapo tarehe 15 ya mwezi wa 7 watumishi wote nataka kuona wamehamia kilolo na kama hawawezi waseme ili tuweze kutafuta watumishi wengine ambao wanaweza kuishi wilayani hapa.
Sendiga amemtaka mkurugenzi huyo bwana Laini kamendu kuhakikisha anapita kaya kwa kaya kuwa himizia wananchi wa Wilaya hiyo wahakikishe wanapanda zao la palachichi ambalo inasadikiwa kuwa limekuwa lina stawi vyema wilayani kilolo.
Mkoa huu ni maarufu kwa kilimo hivyo nawataka wakazi wa mkoa huu hasa wakazi wa kilolo mjikite kulima palachichi kwani kwa sasa zao hili soko lake lipo vizuri alisema sendiga
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.