Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi imetoa mikopo yenye thamani ya milioni 819 kwa vikundi mbalimbali ya vijana, walemavu na wanawake ikiwa ni asilimia 10 ya mapato yake ya ndani.
Mikopo hiyo imekabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe.Queen Sendiga kwa niaba ya Halmashauri hiyo.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhiana mikopo hiyo Mkuu wa Mkoa wa Iringa ameipongeza Halmashauri hiyo ya Mufindi kwa kuzidi malengo waliyojiwekea katika utoaji wa mikopo hiyo na kuzitaka halmashauri nyingine kuiga mfano kutoka kwao.
Aidha Mhe.Queen Sendiga amewataka wale wote waliopewa mkopo huo kuurejesha kwa uaminifu ili na wengine nao wapewe ili kujiletea maendeleo yao na ya Taifa kwa ujumla.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.