Na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa
Mwenge wa uhuru ukiwa mkoani Iringa utazindua, kukagua na kuweka mawe ya msingi miradi ya maendeleo 39 yenye thamani ya shilingi 24,191,060,696.40.
Hayo yalisemwa na mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza alipokuwa akisoma taarifa ya Mkoa wakati wa kupokea Mwenge wa uhuru ukitokea Mkoa wa Mbeya leo.
Masenza alisema kuwa Mwenge wa uhuru ukiwa mkoani Iringa utakimbizwa katika halmashauri tano na kuhimiza na kuhamasisha shughuli za maendeleo. “Jumla ya miradi ya maendeleo 39 yenye thamani ya shilingi 24,191,060,696.40 itazinduliwa, itawekwa mawe ya msingi na kukaguliwa” alisema Masenza. Pamoja na kutembelea miradi ya maendeleo, Mwenge wa uhuru katika maeneo yote utakapokimbiza utatoa ujumbe maalum wa mwaka 2018 usemao ‘elimu ni ufunguo wa Maisha wekeza sasa kwa maendeleo ya taifa letu’.
Masenza alisema kuwa ujumbe wa Mwenge mwaka huu unabeba maudhui muhimu wakati serikali ya awamu ya tano imedhamiria kujenga uchumi wa viwanda. “Ni ukweli usiopingika kwamba ili kufikia adhima hii ni lazima kuwekeza vya kutosha katika elimu ili kuweza kuwa na rasilimali watu wenye ujuzi na maarifa ya kutosha” alisema Masenza.
=30=
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.