Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kuwasili Mkoani Iringa Juni 22,2024 ukitokea mkoani Njombe ambapo utazinduaa miradi yenye thamani ya zaidi ya bilioni 600 na utakimbizwa kwenye Halmashauri 5 za Mkoa wa Iringa.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba Juni21,2024 amewaambia wanahabari kuwa Mwenge huo utapokelwa Mkoani Iringa ukitokea Mkoa wa Njombe ambapo mapokezi yatafanyika kwenye Kijiji cha Nyigo wilaya ya Mufindi na utakagua na kuweka mawe ya msingi miradi 50.
Ambapo Mhe. serukamba amesema kwamba mwenge huo unatarajiwa kukimbizwa umbali wa kilomita 873.03 na baada ya kumaliza mbio zake Mkoa wa Iringa utakabidhiwa mkoa wa Dodoma.
Aidha Mhe. Serukamba amewataka wananchi wote kujitokeza kwa wingi kuupokea na kuulaki mwenge wa uhuru katika mapokezi,barabarani,kwenye miradi na maeneo ya mikesha.
Kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru wa Mwaka 2024 inasema “Tunza Mazingira, na shiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa ujenzi wa taifa Endelevu”
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.