Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba leo Juni,27,2024 amekabidhi mwenge wa uhuru 2024 kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, mara baada ya kumaliza mbio zake za kukagua na kumulika miradi 50 ya Mkoa wa Iringa.
Makabidhiano hayo yamefanyika mapema leo hii kwenye kata ya Chipogolo, Wilaya ya Mpwapwa. Sambamba na hayo Mhe. Serukamba amewakabidhi Vijana Sita ambao ni wakimbiza Mwenge wa Uhuru 2024 waliobeba ujumbe wa Mwenge wa uhuru wa mwaka huu.
#www.kazi.go.tz
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.