Mkuu wa mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba amewaomba wananchi na viongozi wa dini Nchini kuchangia ipasavyo Kwa kutoa mawazo na fikra zao nzuri ili Taifa liweze kupata dira nzuri itakayosaidia kujenga nchi yetu ya Tanzania.
Mhe. Serukamba amezungumza hayo mbele ya mgeni rasmi Mhe. Dkt. Tulia Ackson, spika wa bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji. Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb.),
Akizungumza katika Kongamano hilo Mhe. Serukamba amewajulisha wananchi na viongozi kutambua Mikoa ya Mbeya, Songwe, Njombe na Iringa zina nafasi kubwa sana kwenye nchi hii kwasabau Mikoa hii ndo inayolisha nchi.
"Tunaposema Tanzania inajitosheleza Kwa chakula ni kwa sababu ya mikoa hii minne."
Pia Mhe. Serukamba amesema kuwa Nchi yetu imefanya makubwa sana kuanzia kwenye sekta ya maji,elimu, barabara,Afya, hivyo siku hii ya leo tujipange vizuri tuje na mawazo mapya ya jinsi gani tunaweza kuziboresha zaidi sekta zote hizo kwa maendeleo ya kuanzia sasa mpaka 2050.
Aidha Mhe. Serukamba amesema kuwa katika kipindi hiki kifupi Mambo mengi mazuri na Makubwa ya kujenga nchi yamefanyika ndani ya miaka 3 ya uongozi wa Mhe, Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan chini ya usamizi wa chama Cha mapinduzi.
Kongamano hilo limefanyika katika ukumbi wa Edeni Highland Hotel Mbeya na Kuudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka mikoa ya nyanda za juu.kusini.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.