Mhe. Halima Omary Dendego, Mkuu wa Mkoa Iringa amefunga kikao cha wadau wa misitu mkoani humo Leo hii katika ukumbi wa halmashauri ya Wilaya ya Mufindi. Akiongea ndugu, Injinia Leornad Massanja amesema kuwa kikao hichi ni muhimu sana hasa kwa mustakabali wa uchumi wa Mkoa wetu na Taifa kwa jumla, pia amewataka wadau wa sekta hiyo kufanya biashara kulingana na soko linavyoenenda uko duniani. Mhe Dendego, amewapongeza wadau wa misitu kwa kujitokeza kwa wingi katika kikao hicho na amewataka kuongea hali halisi wanayokabiliana nayo hii itasaidia sana kutatua changamoto zilizopo. " Tunatakiwa kufanya biashara kisasa zaidi ili kupata mapato makubwa kuanzia ngazi wilaya hadi Taifa, na itapelekea kushindana na soko la kitaifa". Mhe Dendego, amefunga Kikao hicho cha wadau wa misitu na mada mbalimbali zinawasilishwa. Kikao kimehudhuliwa na waheshimwa wakuu wa Wilaya zote tatu, kamati za ulinzi
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.