Mhe Halima Omary Dendego, Mkuu wa Mkoa Iringa Leo amefanya ziara ya kukagua shamba la Sao hill ambapo ameona ufanisi mkubwa unaofanywa na wataalamu hao kuendeleza Kilimo cha zao la miti na kupelekea kupata pato kubwa kwa Taasisi na nchi kwa ujumla. " Niwapongeza kwa kutoa miche kwa taasisi mbalimbali za serikali na kwa wananchi wa vijiji jirani hii inasaidia kuongeza kipato kwa jami". Baadae Mhe Dendego, alipata fursa ya kutembelea baadhi ya viwanda na kujionea uchakataji wa zao la miti, akiwa mafinga ametembelea kiwanda cha Rush chanzo na Dazhong, amewapongeza wawekezaji hao kwa kutengeneza ajira na bidhaa nzuri sana
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.