Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe.Halima Dendego amewataka watumishi wote wa Serikali ndani ya Mkoa kufanya kazi bila kuvunja sheria na atakayebainika kwenda kinyume hatua kali ikiwemo kusimamishwa kazi zitachukuliwa dhidi yake.
Dendego ametoa rai hiyo kwenye kikao cha madereva bajaji ambao kupitia kwa mwenyekiki wa bajaji Mkoa wa Iringa ndugu Melabu Kiwhele alieleza adha wanazokutana nazo madereva hao ikiwa ni pamoja na kupigwa,kukimbizwa na gari za polisi pamoja na manispaa kukamata bajaji zao bila utaratibu.
Akitoa msimamo wa Serikali Dendego amesema hakuna aliyejuu ya sheria kuanzia watumishi wa manispaa,jeshi la polisi na madereva hao huku akiwataka kila mmoja kutimiza wajibu wake na atakaenda kinyume na sheria itafuata mkondo wake.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Ndg. Daud Yasin ameliomba jeshi la Polisi kupitia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuandaa mafunzo kwa vijana hao na yeye atalipia leseni za wale wote watakaofuzu katika mafunzo hayo
Imetolewa na Afisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.