Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe Ally Hapi ameanza ziara ya siku moja katika Wilaya ya Mufindi. Baada ya mapokezi katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa alianza ziara katika ofisi ya CCM Wilaya ya Mufindi na kufanya kikao na kamati ya siasa ya Wilaya.
Mhe Hapi aliitaka kamati ya siasa ya Wilaya kudumisha umoja, mshikamano na ushirikiano.
Mhe Hapi alikitaka chama cha Mapinduzi kuendelea kuisimamia serikali katika ngazi zote juu ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM. "Tunatamani chama kiwe jicho la serikali. Tukubaliane kuwa mtu pelee kuiambia ukweli serikali ipasanyo ni chama cha Mapinduzi" alisisitiza mhe Hapi.
Mkuu wa Mkoa alikitaka chama kuwa karibu zaidi na wananchi. Alishauri chama hicho kutosubiri vikao. "Tusiwe chama cha kusubiri vikao tu, lazima tuangalie hali ya siasa sababu siasa ni pana ikihusisha na shida za watu" alisema mhe Hapi.
Katika siku ya pili ya ziara yake, mkuu wa mkoa akiwa wilayani Mufindi ataongea na wafanyakazi na kufanya kikao na wazee.
=30=
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.